WANAFUNZI 417 WAKATISHA ELIMU WILAYANI MLELE-Septemba 27,2017

Na.Issack Gerald-Mlele Katavi
ZAIDI ya wanafunzi 417 wa sekondari katika halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi wamekatisha masomo yao kwa kipindi cha kati ya mwaka 2014 na 2016 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mimba na utoro
Hali hiyo imebainishwa na Afisa elimu idara ya Sekondari Bw.Sylivanus Raphael Kunambi ambapo amesema kuwepo changamoto ya wanafunzi kuikatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo utoro na mimba.
Kunambi amesema kwa mwaka 2014 wanafunzi 108 sawa na asilimia 17.4 ya wanafunzi wote waliokuwa wamesajiliwa katika mwaka huo hawakuhitimu huku mwaka 2015 idadi ya wanafunzi ambao hawakumaliza masomo yao ikiongezeka na kufikia 160 sawa na asilimia 22.9  wakati huo kwa mwaka 2016 wanafunzi 149 sawa na asilimia 20 ya wanafunzi wote waliokuwa wamesajiliwa wakishindwa kuhitimu elimu ya sekonadri..
Aidha ametaja sababu nyingine inayosababisha wanafunzi kutohitimu elimu ya Sekondari ni pamoja na jamii ya wafugaji wanaohama hama katika wilaya ya Mlele hali ambayo inaathiri elimu ya mtoto.

Hata hivyo wazazi,walezi na jamii imeaswa kutambua nafasi na haki ya mtoto kupata haki yake ya elimu kama inavyostahili kwa kuwa ni haki yake.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au Ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA