NDUGU 6 MKOANI RUKWA WAHUKUMIWA KUNYONGWA-Septemba 27,2017

Na.Issack Gerald-Sumbawanga Rukwa
NDUGU sita wa familia moja wamehukumiwa kifo kwa kunyongwa baada ya kuthibitika Kuwa walimuua ndugu yao wakimtuhumu Kuwa ni mchawi.

Ndugu hao walihukumiwa Jana na mahakama kuu ya kanda ya Sumbawanga baada yakuridhika na upande wamashtaka Kuwa walitendakosa hilo.
 Jaji Wa Mahakama hiyo, Dk Adam Mambi alisoma hukumu hiyo ambapo alisema kuwa pasipo kuacha shaka watuhumiwa walifanya mauaji ya ndugu yao huyo. 
Waliokutwa na hatia katika shauri hilo ni Ferdinand Kamande, Peter Mpandisharo, Edes Kamande, Stephen Sikanda, Henrick Nguvumali Anatory Kamande huku watuhumiwa Alistid Kamande na Will broad Kamande wakiachiwa huru kwa kutokutwa na hatia Katika shtaka hilo.
Katika shauri hilo upande wa mashitaka uliongozwa na mawakili wa serikali ambao ni Scolastica Lugongo na Adolf Lema huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na wakili Mathias Budodi, ambapo ilidaiwa kuwa washitakiwa walifanya mauaji hayo Septemba 27, mwaka 2014.
Awali Ilielezwa mahakamani hapo kuwa siku ya tukio nyakati za usiku washitakiwa wakiwa na silaha za jadi kama ambazo ni mapanga, nondo, mawe, majembe walivamia nyumba ya Kamande na kuvunja mlango ambapo Kamande alikimbia kuelekea kusikojulikana. 
Ilielezwa kwamba baada ya hapo waliichoma moto nyumba hiyo na kuteketeza kila kitu kilichokuwemo ndani kisha kuondoka zao. 
Wakati nyumba hiyo ikiteketea kwa moto Kamande aliyekuwa amekimbia ili kunusuru maisha yake, ndipo walipomtafuta na kufanikiwa kumpata na kisha kuanza kumpigwa wakimtuhumu kuwa ni mchawi na baada ya kumpiga waliamua kumchoma moto hadi kufa. 
Ilidaiwa kuwa washitakiwa hao walikamatwa na polisi Oktoba 10, 2014 na baada ya kuhojiwa na polisi walikana shitaka hilo.
Awali kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mawakili wa Serikali waliiomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwani vitendo vya watu kuua wenzao kwamadai Kuwa ni wachawi vimeanza kukithiri mkoani humo.
Akitoa adhabu hiyo Jaji wa Mahakama hiyo, Dk Mambi amesema ameridhishwa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka hivyo kwa kutumia Kifungu cha Sheria ya Makosa ya Jinai Namba 196 Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo 2002 anawahukumu watu hao sita kunyongwa hadi kufa.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au Ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA