CCM WILAYANI MPANDA WAPATA VIONGOZI WAKE JUMUIYA YA WAZAZI,UVCCM NA UWT-Septemba 26,2017

Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
JUMUIYA ya wazazi ya chama cha Mapinduzi CCM Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,imemchagua Bw.Abdalah Mtwenya Kapongolola kuwa mwenyekiti atakayeiongoza jumuiya hiyo mpaka mwaka 2022.

Msimamizi wa uchaguzi huo ambao umefanyika leo mjini Mpanda Bw.Reginald Mhango amewataja wengine waliochaguliwa kuwa ni na Modesta Mpanda Ngazi mjumbe wa mkutano mkuu taifa,Yasin Kilimanjaro mjumbe Halmashauri kuu,Leticia Chindiko Mkutano mkuu wa Mkoa,Michael Nestori Mwakilishi UVCCM mkoa na Bi.Richard Mayaya mwakilishi wa UWT.
Wengine waliochaguliwa uwakilishi baraza la wazazi Wilaya ni Eriziel Samweli Fyula,Simon Malima na Joseph Mpangalilo.
Mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo Bw.Abdalah Mtwenya Kapongolola pamoja na mambo mengine ameomba ushirikiano Kutoka kwa wanajumuiya hiyo ili kuendeleza chama na kutunza rasilimali za chama kwa ajili ya kukuza uchumi wa chama.
Naye katibu wa CCM Wilayani Mpanda Bi.Elizabeth Kasmili Kibiriti amewapongeza wanachama kutumia nafasi zao kuchagua viongozi wanaowataka kwa manufa aya chama huku mwenyekiti mstaafu wa jumuiya hiyo Bw.Abel Hamis Kimazi akiwataka wanachama kushirikiana na viongozi wapya kuendeleza chama.
Jumala ya kata 27 za wilaya ya Mpanda zilizokuwa na wapiga kura zaidi ya 246 zimeshiriki uchaguzi huo huku mkutano ukihudhuriwa na wanachama wa jumuiya hiyo karibu 300 wakiwemo madiwani na mbunge wa jimbo la Nsimbo.
Kata hizo ni Litapunga, Mkanyagio, Magamba, Kanoge, Sitalike, Shanwe, Kazima, Nsimbo, Kapalala, Uwanja wa ndege,  Mwamkulu, Mpanda Hotel, Kashaulili, Ibindi, Kakese,  Ilembo, Kawajense, Uruwila, Machimboni, Nsemulwa, Itenka, Misunkumilo, Kasokola, Ugalla, Mtapenda, Majengo na Katumba.
 Jumuiya nyingine ambazo jana zimefanya uchaguzi ili kupata viongozi wake wilayani Mpanda ni Umoja wa Vijana wa chama cha Mapinduzi CCM (UVCCM) na Umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi CCM (UWT).

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au Ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA