WASAFIRI WANAOTUMIA TRENI KUTOKA MPANDA-TABORA WAOMBA KUONGEZEWA MABEHEWA-Julai 18,2017

Treni ikiwa kituo cha Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald)
Wakazi wa Halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameliomba shirika la Reli Tanzania kuwaongezea mabehewa ya abiria na mizigo ili wasafiri na kufika kwa wakati.

Hayo yamesemwa na baadhi ya wananchi ambao hata hivyo hawakutaka majina yao yatajwe ambapo pia wamesema wakati mwingine wasafiri hukosa tiketi na kujikuta kiti kimoja kikikatiwa tiketi na zaidi ya watu wawili.
Kwa upande wa mkurugenzi wa Shirika la Reli Masanja Kadogosa amekiri kuwepo kwa tatizo hilo ambapo amesema wanalitafutia ufumbuzi ili wasafiri wapate huduma katika hali nzuri.
Usafiri ni moja ya mambo yanayochangia kukua kwa uchumi kwani watu hutoka sehemu moja kwenda nyingine na mazao husafirishwa pia kwa njia hiyo.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA