UCHOMAJI NYUMBA ZA WAKAZI WA KATA YA LITAPUNGA HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO MKOANI KATAVI,WANANCHI WALALAMIKA,MBUNGE ALAANI TUKIO HILO,JESHI LA POLISI KATAVI LASEMA LINA TAARIFA YA OPARESHENI HIYO KUFANYIKA LAKINI LIMEKANA KUWEPO KWA UCHOMAJI MOTO NYUMBA-Julai 25,2017

Baadhi ya Wakazi wa kata ya Litapunga iliyopo halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wamelalamikia zoezi la kuondolewa katika maeneo yanayodaiwa kuwa hifadhi ya misitu kwa kuchomewa nyumba zao.

Wakizungumza na Mpanda radio asubuhi ya leo,wamesema kuwa awali Shirika kuhifadhi na kutunza mbuga za wanyama Tanapa ilitoa siku saba kwa wananchi kuyahama makazi ambapo Mbunge wa jimbo la Nsimbo Mh.Richard Mbogo alidai kuwa hazitoshi kwa suala hilo.
Akizungumza na Mpanda Radio kwa njia ya akiwa safarini Dar ess Salaam,amekili kuwepo kwa suala hilo  na kulaani kitendo cha kuchoma makazi hayo huku akiitaka kamati ya ulinzi ya wilaya kuheshimu haki za binaadamu.
Kwa upande wa Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Katavi Damasi Nyanda amethibitisha kuwepo kwa oparesheni hiyo huku akikana kuwepo kwa vitendo vya uchomaji wa makazi hayo pamoja na mazao.

HABARIKA NA P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA