SAFARI YA TRENI MPANDA-TABORA YAENDELEA BAADA YA AJALI ILIYOSABABISHA MABEHEWA KUDONDOKA-Julai 25,2017

Treni inayosafiri kutoka Mpanda Mpaka Tabora (PICHA NA.Issack Gerald)

WASAFIRI wanaotumia usafiri wa Treni kutoka Mpanda kuelekea Tabora jana wameanza safari baada ya kukwama tangu juzi kwa kile kinachoelezwa kuwa juzi kulitokea ajali iliyosababisha mabehewa ya mizigo kuanguka.

Wasafiri hao wakiwemo Moshi Kisenge,Asha Mashaka na Abubakari Ramadhani wamesema licha ya kupoteza muda wakisubiri safari,kwa sasa wanajisikia furaha baada ya kupata uhakika wa safari yao.

Hata hivyo Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Mkoani Katavi Vivian Venas haukuwa tayari kuzungumza na Mpanda Radio kuhusu mkwamo wa safari ya Treni,zaidi ya kusema kuwa tangu asubuhi anahangaika na safari ya treni.

Mapema leo asubuhi,baadhi ya wafiri wakiwa hawajui hatima ya safari kutokana na mkanganyiko wa ratiba ya treni kuondoka,Wasafiri hao wakiwemo Grace Ndaiso,Marco Peter na Ester Abel wakizungumza na Mpanda Radio katika kituo cha Treni Mpanda pamoja na mambo mengine walikuwa wamesema wasafiri wasiokuwa na pesa ya ziada wamepata adha ya njaa.

Kwa mjibu wa ratiba ya Treni kutoka Mpanda kuelekea Tabora, ilitakiwa iwe imeondoka tangu jana majira ya saa tisa alasiri ambapo mamia ya abiria wakiwa na mizigo yao mpaja jioni ya leo walikuwa hawajui hatima ya safari yao.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA