RAIS MAGUFULI AUNGANA NA WATANZANIA KUYAOMBEA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA-Julia 25,2017

Rais John Maguli akikata utepe kuashirika kuzindua barabara ya lami ya Manyoni-Itigi kwa kiwango cha lami(picha na Mtandao)
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Pombe Magufuli,amesema katika kuadhimisha siku ya mashujaa inayoadhimishwa Julai 25 ya kila mwaka,unaungana na watanzania wote kuyakumbuka majeshi yote yaliyopigania na wanaoendelea kupigani amani ya nchi na kuifanya Tanzania kuwa kimbilio wa watu wengi.

Rais Magufuli aetoa kauli hiyo akiwa Mkoani Singida katika ziara ya kufungua mradi wa barabara ya Manyoni – Itigi yenye urefu wa kilometa 89.3 iliyojengwa kwa kiwango cha lami.
Rais Magufuli ambaye amewasili Mkoani Singida akitokea Mkoani Tabora amesema ataendelea kushughulikia matatizo ya wananchi kila yanapojitokeza.
Jumla ya barabara zilizojengwa kwa kiwango cha lami zenye urefu wa kilomita zaidi ya 700 na kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 816 zimefunguliwa na kuwekewa mawe ya msingi tangu alipoanza ziara katika miko ya Kigoma,Kagera,Tabora na Singida.

Habari zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA