MADIWAMI HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA WAAGIZWA KUSIMAMIA USAFI WA MASOKO-Julai 25,2017

Kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Mh.Hamad Mapengo(PICHA Kwa hisani ya Mtandao
MADIWANI wametakiwa kuhakikisha masoko yaliyopo katika Halmashauri zao yanafanyiwa usafi ili wafanyabiashara watoe ushuru kwa wakati na bila shida.

Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mh.Hamad Mapengo katika kikao cha baraza la madiwani ambacho kimefanyika katika Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda.
Mh.Mapengo amesema masoko yasipofanyiwa usafi yanasababisha migogoro isiyo ya lazima miongoni mwa wadu wanaotegemea masoko hayo.
Katika hatua nyingine,Madiwani katika Halmshauri hiyo wametakiwa kutatua migogoro ya mipaka katika maeneo yao ili wananchi waishi kwa amani bila matatizo.
Hata hivyo kupitia kikao cha leo cha baraza la madiwani,imeagizwa kuwa ushuru unaotolewa na wafanyabiasahara lazima utumike kusafisha masoko ili mazingira yawe safi na kulinda afya za wanaotumia masoko hayo.

Habarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA