MKUU WA MKOA WA KATAVI KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UANZISHWAJI BENKI YA WANANCHI.


Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga  leo anataraji kukutana na kuzungumza na vyombo vy ahabari ili kueleza mikakati ya uanzishwaji wa benki ya Wananchi Mkoani Katavi.
Ofisi za mkuu wa Mkoa(PICHA NA.Issack Gerald

Taarifa ya Mkuu wa Mkoa ambayo imetolewa na Katibu wa Mkuu wa Mkoa,inaeleza kuwa kikao hicho kinataraji kufanyika majira ya saa tano Asubuhi.
Wiki iliyopita wakati akipanga kuzungumza na waandisahi wa habari,alisema kuwa benki hii malengo yake ni kumwinua kiuchumi mwanakatavi sanjari na kuongeza mapato ya mkoa kwa kuwa benki hii itatumiwa na wanakaziu wa mkoa wa katavi.
Mpaka kufikia wiki iliyopita,Mkuu wa Mkoa alisema kuwa kuna kiasi cha shilingi bilioni 3.2 za kuanzia kama salio katika akaunti ambapo pia na jengo itakapokuwa benki hiyo limekwishapatikana.
Hata hivyo taarifa rasmi inatarajiwa baada ya mkuu wa mkoa kuzungumza na waandishi wa habari.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM   

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA