MKOA WA KATAVI KUANZISHA BENKI YA WANANCHI


Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi
Mkoa wa Katavi umepanga kuanzisha benki ya wananchi kwa ajili kurahisisha na kuharakisha maendeleo ya wakazi wa Mkoa wa Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake (hawapo pichani) kuhusu uanzishwaji wa benki ya wananchi(PICHA NA.Issack Gerald)
Mwenyekiti wa kamati ya Waratibu wa Benki ya wananchi Mkoa wa Katavi
                             

Akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake,Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga amesema kuwa benki hiyo inatarajia kuanza kazi yake ifikapo Mwezi Aprili 2017.
Amesema kuwa katika mkutano unaotarajia kufanyika Kesho Julai 27 na kushirikisha wadau mbalimbali,amewataka wananchi kujitokeza kutumia fursa ya uwepo wa benki hiyo kijkwamua kiuchumi.
Aidha Jenerali Muhuga amesema katika kuanzisha benki kunahitajika kiasi cha shilingi Bilioni 3 kwa ajili ya usajili,jengo na kianzio katika akaunti.
Kwa upande wake Mhandisi Awariywa Nnko Mwenyekiti wa kamati ya Waratibu Benki ya Wananchi mkoani Katavi ambaye pia ndiye Katibu tawala Msaidizi kitengo cha Uchumi na Uzalishaji kutoka Ofisi ya Mkoa wa Katavi amesema miongoni mwa wadau ambao wamealikwa kushiriki katika kikao cha kesho ili kuchangia fedha za uanzishwaji wa benki hiyo ni pamoja na mameneja wa Benki Mkoani Katavi,mameneja wa vyama vya ushirika mkoani Katavi,viongozi wa dini,vyama vya siasa,Chama kikuu cha Ushirika LATCU na waandishi wa habari.
Mkoa wa Katavi unaanzisha  Benki ya wananchi kwa kushirikiana na Jumuiya Ya Benki za Wananchi Tanzania-Community Banks Association of Tanzania (COBAT) huku lengo zaidi likiwa ni kupata uelewa pamoja na utaratibu kuhusu manufaa ya kuwa na  benki ya wananchi katika Mkoa wa Katavi.
Mpaka sasa jumla ya Mikoa 8 ya Tanzania imekwishaanzisha benki ukiwemo mkoa wa Kilimanjaro na Kagera.
Jumla ya wadau wapatao 400 wanatarajia kushiriki katika Mkutano huo.
Msimamizi mkuu wa benki ya wananchi Mkoani Katavi ni waziri mkuu mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne Mh.Mizengo Kayanza Peter Pinda
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
                                  

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA