MBUNGE VITI MAALUMU MPANDA AMWAGA MSAADA WA FEDHA NA BAISKEL KWA WANAWAKE

Wanawake wajasiliamali wakiwa katika mkutano na mbunge viti maalumu Mh.Anna Lupembe(PICHA NA.Issack Gerald)
                                       
Mbunge viti maalumu akizungumza na wanawake wajasiliamali katika viwanja vya shule ya Msingi Kashato(PICHA NA.Issack Gerald)
                                     

MBUNGE wa Wakati huo huo Mh.Anna Lupembe amekabidhi Shilingi milioni 4 kwa vikundi 40 kati ya 80 vya wanawake  alivyoviunda na kuvipatia elimu ya ujasiliamali Aprili mwaka huu.

Fedha hiyo ameikabidhi kwa wanawake hao katika mkutano ambao ameufanya akiwa na wanawake hao katika viwanja vya shule ya Msingi Kashato Mpanda Mjini.
Amesema kuwa vikundi vingine 40 ambavyo havijapatiwa fedha hiyo ili kuanzisha miradi ameahidi kuwapatia fedha hiyo mwezi Septemba mwaka huu.
Katika vikundi hivyo kila kikundi kimepatiwa shilingi laki moja.
Katika hatua nyingine Mbunge huyo amekabidhi baiskeli tatu kwa wanawake wenye ulemavu mmoja akitokea Manispaa ya Mpanda na wawili Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo.
Aidha mbunge huyo ameahidi kuendelea kuwasaidia wanawake wajasiliamali watakaokuwa wameonesha kuzitumia vizuri fedha wanazopatiwa ili kuanzishia miradi ya maendeleo.
Hata hivyo amewataka wanawake kuwa wamoja kwa kupendana na kusaidiana katik ashida mbalimbali na kuacha malumbano yasiyokuwa na tija kwao.
Nao baadhi ya wanawake waliopatiwa fedha hiyo wamempaongeza mbunge wao kwa kuendelea kutekeleza ahadi alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015.
Mpaka sasa kuna vikundi vinmgi vya wajasiliamali Mkoani Katavi ambavyo vimekwisha patiwa elimu ya ujasiliamali ambapo kinachosuburiwa na namna ya kusaidiwa ili kupunguza ugumu wa maisha.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA