BALAZA LA MADIWANI LAOMBA SHERIA ZA ZIMAMOTO KUPITIWA UPYA,MBUNGE VITI MAALUMU PAMOJA NA MAMBO MENGINE KULISEMA BUNGENI.


Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi
BARAZA la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi limeliomba jeshi la zimamoto na uokoaji  Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi kupitia upya sheria inayomtaka mwananchi kuchangia kiasi kikubwa cha fedha ukilinganisha na uwezo wa mwananchi kumudu gharama hizo kwa mwaka.
Wataalamu mbalimbali katika Manispaa ya Mpanda wakishiriki kikao cha mwaka cha Baraza la madiwani Manispaa ya Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald)


Ombi hilo limetolewa na madiwani wapatao 22 wanaounda baraza hilo kupitia mkutano mkuu wa kufunga mwaka wa fedha 2015/2016 mkutano ambao umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
Aidha Baraza limebaini kuwa mwananchi huchangia kuanzia shilingi laki moja na nusu(150,000/=) kwa ajili ya gharama za kujikinga na majanga ya moto huku kiwango hicho kikitajwa kuwa kikubwa huku wananchi wakionekana kutokuwa na elimu ya kutosha ya kujikinga na majanga ya moto.
Mara kwa mara wakazi wa Manispaa ya Mpanda wamekuwa wakilalamika kutozwa kiasi kikubwa cha pesa huku jeshi la Zimamoto na uokoaji wakilalamikiwa kuchelewa wakati wa majanga ya moto
Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu(CCM) Mkoani Katavi Mh.Anna Lupembe amesema kupitia vikao vya bunge vinavyotarajia kuanza mwezi Septemba mwaka huu, atawasilisha ombi hilo la Halmashauri kutaka wananchi wapunguziwe gharama za uchangiaji ziamoto ili kupunguza mzigo mkubwa kwa mwananchi wa maisha ya kawaida.
Mbunge viti maalumu mkoani Katavi Mh.Anna Lupembe akichangia hojakatika kikao cha mwaka cha Baraza la madiwani Manispaa ya Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald)
                         
Hata hivyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Mh.Willium Mbogo amesema kuwa hata Halsmashauri haina ufahamu wa kutosha wa namna Zimamoto na Uokoaji wanavyoendesha shughuli zao na kutoza kiwango hicho cha pesa katika Manispaa.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa sasa lipo chini ya Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi baada y akuondolewa katika mamlaka ya Halmshauri miaka ya hivi karibuni.
Katika hatua nyingine Mh.Lupembe amesema suala la upimaji wa uzito wa mazao ataliwasilisha bungeni ili kupata ufafanuzi na utatuzi wa vipimo halisi ikiwa mazao yanatakiwa kupimwa kwa kilogramu 75 au 100 kwa kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa wakiendelea kudidimia katika umaskini kutokana na kuuza katika vipimo vinavyowakanganya nje ya matumizi ya rumbesa.
Hatu ya kujadiliwa kwa vipimo halisi vya mazo imefanyika ikiwa ni baada ya wakulima kulalamika kunyanyaswa katika upimaji wa mazao.
Hata hivyo ajenda nyingine ambazo zimejadiliwa ni zile zinazohusu sekta ya maji,umeme.afya,elimu,maambara na suala la madawati
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA