MKOA WA KATAVI WABAKIZA MADAWATI 2108 KUMALIZA TATIZO LA MADAWATI SHULENI,MKUU WA MKOA ASEMA KIKOMO CHA TATIZO JULAI 31 MWAKA HUU.


Mkoa wa Katavi umekamilisha madawati 13915 kati ya madawati 15452 yanayotakiwa kukamilisha idadi ya madawati yatakayokuwa yakikidhi idadi ya wanafunzi kwa shule za msingi ambapo mpaka sasa uhaba wa madawati kwa Shule za Msingi Mkoani ni madawati 1537.
Sehemu ya madawati 327 yaliyokabidhiwa na wabunge Manispaa ya Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald)
Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga  baada ya kupokea msaada wa madawati 146 kutoka kwa mbunge wa viti maalumu Mkoani Katavi Mh.Anna Lupembe ambapo madawati hayo yaliyotokana na Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA makabidhiano ambayo yamefanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Kashaulili.
Jenerali Muhuga pia amesema kuwa upungufu wa madawati kwa shule za sekondari ni madawati 571 ambapo yaliyokwishakutengenezwa ni madawati 1642 huku jumla ya madawati yanayotakiwa yakiwa  madawati 2213.
Katika hatua nyingine Mbunge huyo wa viti maalumu amechangia bati zenye thamani ya shilingi milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya Msingi Nsemulwa iliyopo Manispaa ya Mpanda yenye zaidi ya wanafunzi 2500 wakiwemo zaidi ya 800 wa darasa chekechea na darasa la kwanza huku vyumba vya madarasa vikiwa 7 ambapo kwa uwiano wa wanafunzi waliopo ukilinanisha na walimu waliopo,kila mwalimu analazimika kufundisha wanafunzi 200.
Mbunge viti Maalumu(CCM)Mpanda Mjini baada ya kukabidhi madawati(PICHA NA Issack Gerald)
                            
Kwa upande wake Mbunge wa Mpanda Mjini Mh.Sebastian Simon Kapufi amechangia madawati 181 ambayo nayo yamekabidhiwa jana kwa mkuu wa Mkoa ambapo hata hiyo baada ya kuchaguliwa,mwanzo mwa mwaka huu,kila kata ya Manispaa aliipatia shilingi milioni moja kwa ajili ya utengenezaji wa madawati.
Aidha pamoja na kuwapongeza wakazi wa Mkoa wa Katavi kwa kuwa na moyo wa kuchangia maendeleo katika miradi mbalimbali,mkuu wa Mkoa pia amesema kuwa madawati yote yanatarajia kukamilika ifikapo Julai 31 mwaka huu.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM   

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA