WANAWAKE WANAOUZA MIILI YAO MPANDA WATAKIWA KUFIKA OFISI YA MKUU WA WILAYA KUPATA MBINU YA UJASILIAMALI KUEPUKA MAZINGIRA HATARISHI WALIYONAYO



WANAWAKE  Wanaofanya biashara ya Kuuza Miili yao  Maarufu kama (Dada poa) Mjini Mpanda  wametakiwa Kufika Katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda ili Wapatiwe Mbinu za Kuunda Vikundi Vitakavyowawezesha Kuinua Uchumi ili kuwawezesha  Kuachana na biashara hiyo.

Kauli hiyo imetolewa  leo na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mh,Pazza Mwamlima wakati akizungumza na Mpanda fm ambapo amesema ofisi yake iko tayari kuwasaidia kwa kuwapa Mikopo ili waachane na Biashara hiyo ambayo Kisheria ni haramu.
Mh,Pazza amesema endapo watakuwa tayari ofisi yake itawasaidia Kwa kuwapa Mafunzo ya Ujasilia Mali kwa kuwatumia Maafisa Maendeleo ikiwa ni Pamoja na kuwapa Mikopo ya Kufanyia biashara.
Uamuzi huo wa Mkuu wa Wilaya umetokana na tukio la hivi Karibuni la baadhi ya Dada poa   Kuiomba Serikali Kuwapa leseni ya Kuitambua Biashara yao ili Waisaidie Kukuza Uchumi wa Nchi kwa Kulipa Kodi Kama Sehemu ya Kuunga Mkono Kauli ya Rais ya hapa Kazi tu.
Mwandishi:Meshack Ngumba
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA