SAUTI YA BUNGENI DODOMA KUHUSU HALMASHAURI YA WILAYA MPIMBWE MKOANI KATAVI


Serikali imesema kuwa imetenga kiasi cha shilingi milioni 246 kwa ajili ya matengenezo ya Barabara za Halmshauri ya Wilaya ya Mpimbwe zenye urefu wa KM 42 kwa kiwango changalawe kwa mwaka wa fedha 2015/2016.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri wa Tawala za mikoa na Serikali za mitaa TAMISEMI Mh.Suleiman Jafo,wakati akijibu swali la mbunge wa jimbo la Kavuu Mh.Pudensiana Kikwembe aliyekuwa akiuliza swali lililokuwa likihoji kuwa,serikali ina mpango gani na barabara zilizopo katika Hamshauri Mpya ya Mpimbe ili kuondoa adha wanazozipata wananchi wanapohitaji kusafiri kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.
Aidha Waziri Jafo amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2016/2017 serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni 324.3 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo ya barabara za changalawe zenye urefu wa KM 49.8 pamoja na matengenezo ya sehemu korofi katika Halmashauri hiyo.
Wakati huo Waziri Jafo akijibu swali la nyongeza la Mh.Pudensiana Kikwembe ,pamoja na mambo mengine amesema kuwa Shilingi bilioni zipatazo 45 zimetengwa katika kutengeneza maeneo korofi yanayounganisha Halmshauri mbalimbali hapa nchini.
Mwandishi :Issack Gerald Bathromeo
Mhariri :Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA