SAUTI YA BUNGENI DODOMA KUHUSU MAKAZI MAPYA YA KATUMBA MKOANI KATAVI


Raia wapya wa Tanzania wanaoishi Katika Makazi ya Katumba wanatarajia Kufanya Uchaguzi wa Viongozi wa  Serikali za Mitaa Mwaka huu ikiwa Mandalizi yameanza Kufanyika.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri ofisi ya rais tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Seleman Jafo wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mh,Richard Mbogo lililohoji ni lini Serikali itatenga fedha za Kukamilisha Uchaguzi wa Serikali za Vijiji na Mitaa Katika Kambi ya Katumba ambayo sasa ni Makazi ya raia hao wapya wa Tanzania.
Kwa Mjibu wa Naibu waziri wa Tamisemi Katika Kata ya Katumba Kuna Vijiji 14 na Vitongoji 51 ambavyo havikufanya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2014.
Mh Jafo amesema uchaguzi haukufanyika kwa sababu ya kuwepo kwa wakimbizi ambao walikuwa hawajapewa uraia wa Tanzania kwa Mjibu wa Sheria za Nchi.
Ili Kukamilisha Uchaguzi huo tayari serikali katika bajeti yake imetenga shilingi Milioni 3.3 ilikuwezesha Uchaguzi huo Kufanyika.
Katika hatua nyingine Mbunge Mbunge wa Nsimbo Richard Philip Mbogo amehoji zaidi ni kwa namna gani Serikali itashirikiana na Shirika la Wakimbizi Duniani UNHCR katika kutatua chanamoto za elimu,maji na barabara zinazowakabili wakazi wa makazi hayo ambapo serikali imesema kuwa inaendelea  na utarartibu kupanga utaratibu wa kuwasiadia.
Wakati huo huo mbunge viti maalumu jimbo la ULYAKULU Mh.Mwaine Jumanne akauliza kuwa kwa kuwa tatizo lililopo la kutofanyika kwa uchaguzi Katumba ni sawa na lililopo jimboni kwake Ulyankulu,ni lini uchaguzi utafanyika,swali hili pia likijbiwa na Naibu waziri ofisi ya rais tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Seleman Jafo amesema kuwa mchakato utaendelea wa maandalizi ya uchaguzi katika kata 3 zilizosalia baada ya eneo hilo kurudishwa katika mamlaka ya TAMISEMI kwa kuwa sasa mmiliki wa eneo hilo yupo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
Mwandishi :Issack Gerald Bathromeo
Mhariri :Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA