HAKIMU MFAWIDHI MAHAKAMA YA WILAYA MPANDA ATOA WITO KWA WAKAZI MKOANI KATAVI KUEPUKA KUFANYA VITENDO UHARIFU



WANANCHI Mkoani Katavi wametakiwa kutofanya vitendo vya uhalifu ili kuepuka  madhara ambayo yatapelekea  kufungwa endapo  watabainika na makosa.

Wito huo umetolewa na hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya mpanda Bw.chiganga Tengwa wakati akizungumza na kipindi cha  kumekucha Tanzania cha Mpanda Radio Fm mapema hii leo.
Mh Chiganga amesema elimu ya kutosha inaendelea kutolewa kwa wananchi kuhusiana na makosa na  adhabu zake ili kuweza kupunguza msongamano wa watu ambao wanafanya makosa mbalimbali.
Aidha amesema watu wengi wamekuwa wakipoteza haki zao za msingi kutokana na kutojua sheria za nchi na kuwasihi wananchi kujua sheria hizo kwani  kwa kutofanya hivo ni kosa kisheria.
Mwandishi:Meshack Ngumba
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA