AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA WIZI WA SIMU MPANDA


MTU mmoja amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo Mjini  Mpanda   kwa  Kosa    la wizi wa simu  zenye thamani ya shilingi laki tatu.

Akisoma shitaka hilo hakimu mkazi wa mahakama hiyo  Mh,Sylvesta Makombe  amemtaja mshtakiwa kuwa ni Ally Wambura (23) mkazi wa Nsemulwa manispaa ya Mpanda.
Amesema mshtakiwa ametenda kosa hilo mnamo Mei 2 mwaka huu maeneo ya Buzogwe ambapo aliiba simu aina ya nokia na tecno pamoja na fedha taslimu kiasi cha shilingi elfu hamsini ambazo ni mali ya Sara Kakoso mkazi wa Kawajense mjini  Mpanda.
Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda Kosa hilo ambapo Mahakama imeahirisha shtaka hilo hadi litakapo tajwa tena Mei 30 mwaka huu kwa ajili ya kutoa hukumu.
Mwandishi :Rogathe Tweve
Mhariri :Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA