WATATU WAFIKISHWA MAHAKAMANI MPANDA KWA TUHUMA ZA SHAMBULIO.


Na.Gervas Boniventure-Mpanda
WATU watatu wamefikishwa katika mahakama ya mwanzo  Mjini Mpanda Mkoani Katavi kwa kosa la kumshambulia Abdala hamissi kwa kumpiga na kumsababishia maumivu makali.

Akisoma shitaka hilo mbele ya mahakama hiyo,mwendesha mashitaka  wa mahakama ya mwanzo Bi.Elly neema, amewataja washitakiwa hao kuwa ni Ramadhani hamisi na Mohamed mussa wakazi wa nsemulwa pamoja na Maneno shabani ambaye ni mkazi wa mikocheni Mjini Mpanda.
Bi.Neema ameiambia mahakama kuwa,mnamo Januar 14 mwaka huu saa moja asubuhi washitakiwa walimshambulia Abdala hamisi kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu makali
Kutokana na shitaka hilo washitakiwa wamekana shitaka dhidi yao na hakimu wa mahakama hiyo Bw.David Mbembela ameahirisha kesi hiyo mpaka itakaposikilizwa tena machi 2 mwaka huu.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA