MTOTO MWENYE MIAKA 4 ACHOMWA MOTO NA BABA YAKE MZAZI KWA TUHUMA YA KULA MBOGA YOTE AINA YA CHAINIZI,POLISI WAMTIA MBARONI KUFIKISHWA MAHAKAMANI MUDA WOWOTE.


Na.Issack Gerald-Mpanda
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Emmanuel Joseph (31) mkazi wa Kata ya Kazima Wilayani Mpanda Mkoani Katavi anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Katavi kwa tuhuma za kumchoma kwa moto mtoto wake aitwaye George Emmanuel(04) akituhumiwa kula mboga aina ya Chainizi.
                                                 
Mtoto wa miaka 4 aliyechomwa  moto na baba yake baada ya kula mboga aina ya chainizi.(PICHA NA.Issack Gerald)

Kamanda Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi ACP Rashid Mohamed,alisema tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 20.02.2016 majira ya saa kumi na moja jioni  maeneo ya Kazima Kichangani Kata ya Kawajense Tarafa ya Kashaulili Wilaya ya Mpanda Mkoa wa katavi
ACP Mohamed alisema kuwa mtoto huyo alichomwa moto vidole vyake vya mkono wa kushoto na baba yake mzazi baada ya mtoto huyo kula mboga yote ya majani aina ya chainizi.
Bw.Emmanuel Joseph aliachana na mke wake Semsin Jahala tangu mwezi wa tatu mwaka jana na kumwacha na watoto watatu.
Taarifa ya kamanda imefafanua kuwa mtuhumiwa alipika ugali pamoja na mboga aina ya chainizi ambapo walikula mchana pamoja na watoto wake na kisha kubakiza kwa lengo la kula jioni ambapo baada ya kula aliondoka na kwenda kwenye majukumu yake ya kila siku ya utafutaji. Aliporudi nyumbani majira ya saa kumi na moja jioni kwa lengo la kuandaa chakula cha jioni ndipo alipobaini mtoto wake huyo amekula mboga yote kitendo kilichopelekea kumpiga na kisha kumchoma moto vidole vyake vitatu vya mkono wa kushoto.
Hata hivyo Mtoto George Emmanuel  amepelekwa katika hospitali ya Wilaya Mpanda kwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
Mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi anatoa wito kwa wazazi/walezi wenye tabia ya kuwanyanyasa watoto kwa namna yoyote ile kuacha mara moja tabia hiyo na badala yake watimize majukumu yao kwa kuwatimizia mahitaji yote ya msingi wanayopaswa kupatiwa watoto wao ikiwa ni sambamba na kuepuka kujichukulia sheria mikononi.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA