JELA MIEZI 4 KWA WIZI WA SIMU MBILI


Na.Gervas Boniveture-Mpanda
Mahakama ya mwanzo  mjini Mpanda imemhukumu mtu mmoja kwenda jela miezi minne au kulipa faini ya shilingi laki moja baada ya kupatikana na kosa la wizi wa simu mbili zenye  thamani ya shilingi laki mbili.

Akisoma hukumu  hiyo jana,Hakimu wa mahakama hiyo Bw. Robert Nyando amemtaja mshitakiwa kuwa ni Abass  Philemon (21) mkazi wa Kawajense mjini Mpanda mkoani Katavi.
Mlalamikaji Agnes Mahanga ameieleza mahakama hiyo kuwa  mnamo tarehe 31 Januari mwaka huu saa 4 asubuhi  mshtakiwa alifika nyumbani kwa Agnes Mahanga wakawa wamekaa baadae mshitakiwa alimuomba cm kwa lengo la kuiangalia,baada ya kumpa cm hiyo agnes alitaka kwenda dukani kununua mafuta ya taa ndipo mshitakiwa akaomba amfatie hayo mafuta.
Mshtakiwa alienda dukani huku akiwa na cm ya agnes mahanga aina ya vodaphone yenye thamani ya sh laki moja na hamsini na cm ya shahidi wake aina ya Tecno yenye thamani ya sh elfu hamsini  BILA ya yeye kufahamu,mshitakiwa hakurudi kutoka dukani ndipo agnes mahanga alipogumdua kuwa mshitakiwa ameondoka na cm yake.
alipoanza kumfatilia kwa kushirikiana na shahidi waliekuwa wamekaa nae pindi mshitakiwa huyo anafika nyumban hapo lakini hakufanikiwa kumpata’
Ndipo mlalamikaji alipotoa taarifa hiyo katika jeshi la polisi na kufanikiwa kumkamata mshitakiwa huyo.
Baada ya kusomewa shtaka hilo Mshtakiwa amekiri kosa na mahakama hiyo kutoa hukumu ya kifungo cha miezi minne au kulipa faini ya shilingi laki moja ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA