WANAFUNZI 523 KATI YA 930 WAFAULU MTIHANI MANISPAA YA MPANDA,130 MATOKEO YAO YAZUILIWA KWA KUSHINDWA KULIPA ADA


Na.Vumilia Abel-Mpanda
JUMLA ya wanafunzi 523 kati ya 930 waliofanya mtihani wa taifa kidato cha nne katika Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda wamefaulu.
                                             
Miongoni mwa wanafunzi waliohitimu mwaka 2015 katika shule ya Sekondari Mwangaza Manispaa ya Mpanda (PICHA NA Issack Gerald)



Wanafunzi wa kike Mpanda waliohitimu mwaka 2015

Takwimu ya ufaulu huo umetolewa na Bi. Eneliya lutungulu  ambaye ni Afisa elimu idara ya elimu sekondari Manispa ya Mpanda wakati akizungumza na Mpanda Radio kwa njia ya simu.
Hata hivyo amesma kuwa matokeo ambayo yamepokelewa mpaka sasa ni ya wanafunzi 800 huku matokeo ya wanafunzi 130 yakizuiliwa kwa sababu ya kuchelewesha ada ya mtihani huo.
Bi.Lutungulu amesema kuwa ufaulu kwa mwaka 2015 umeshuka kwa asilimia 65.4 ukilinganisha na ufaulu wa asilimia 69 kwa mwaka 2014.
Aidha Bi. lutungulu ameitaka jamii kutowaachia majukumu ya kifamilia watoto wao kwa kuwa ni moja ya chanzo kinachosababisha utoro wa rejareja na kupelekea matokeo mabaya katika masomo yao na taifa kwa ujumla.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA