WAZIRI MKUU MAJALIWA AAGANA NA BALOZI WA NAMIBIA,AKUTANA NA BALOZI WA FINLAND NCHINI.


Na.Issack Gerald-Katavi
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekuatana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Namibia ambaye anamaliza muda wake, Bwana Japhet Isaack.
                                                                          
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na balozi Namibia nchini, Mhe. Japhet Isaack ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Januari 8, 2016

Akizungumza na Balozi  Isaack leo ,ofisini kwake ,Magogoni jijini Dar es salaa, Waziri Mkuu ameshukuru Balozi huyo na  kumumwomba  waendeleze uhusiano mwema   ulipo baina ya nchi hizi mbili ambao ulianza tangu enzi za kugombania uhuru ili  kusaidia kukuza uchumi wa nchi hizi mbili.
“Namibia ni  nchi yenye uchumi uanaokua haraka, na mmefanikia katika baadhi ya sekta , hivyo ningependa  Tanzania ijufunze kutoka kwenu hasa katika sekta za Utalii, Afya, na Elimu,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Pia, alitumia fursa hiyo kuwakaribisha  raia wa Namibia kuja kuwekeza nchini  katika maeneo mbalimbali ikiwemo  viwanda  na kuendeleza maeneo ya ukanda maalum ya uwekezaji (EPZ) ili kuongeza thamani ya mazao pamoja na kutatua tatizo la ajira nchini.
Kwa upande wake,  Balozi  Isaack  amesema kwa kipindi alichokaa Tanzania amejifunza mengi, na amefurahishwa  ambavyo Waziri Mkuu pamoja Serikali kwa ujumla  inavyofanyakazi kwa kasi na kwa mafanikio makubwa.
“Hongera, ninafurahishwa na unavyofanya kazi  hongera sana”, alisema Balozi Isack. Pia, amefurahi sana kipindi chote alichokaa Tanzania kwani kimekuwa na matukio mengi yenye  kumbukumbu  nzuri kwake.
Balozi Isack   ameomba mahusiano ya nchi hizi mbili yaendelezwe ili zishirikiane zaidi katika masuala mbalimbali ya kukuza uchumi.
WAKATI HUO HUO,WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Finland nchini, Bwana Pekka Hukka.
                                                                   
Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na balozi wa  Finland nchini Tanzania Mhe. Pekka   Hukka  kabla ya mazungumzo yao ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Januari 8, 2016
Akizungumza jana na Balozi  Hukka,alipomtembelea ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es salaam, Waziri Mkuu amemshukuru Balozi huyo kwa namna ambavyo nchi ya Finland imeendelea kuisaidia Tanzania na  kumumwomba  waendeleze uhusiano mwema uliokuwepo kwa zaidi ya miaka 50 sasa.
“Ninashukuru na kutambua mchango wa nchi yako wa  kuisaidia  Tanzania katika sekta mbalimbali  ikwemo  Utalii na Biashara, ninashukuru sana kwa hilo” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Pia, alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kutoka Finland kuja kuwekeza katika sekta ya viwanda   na kuendeleza maeneo ya ukanda maalum ya uwekezaji (EPZ) ili kuongeza thamani ya mazao pamoja na kutatua tatizo la ajira nchini.
Waziri Mkuu, pia ameendelea kwa kusema Serikali imedhamiria kukusanya mapato kikamilifu na kuzuia mianya ya upotevu wake, hivyo ameiomba Serikali ya Finland isaidie katika kujenga uwezo wa namna bora zaidi ya utekelezaji wa  dhamira  hiyo, kwa kuwa Finland ni kati ya nchi zenye mifumo bora na madhubuti ya ukusanyaji wa mapato.
Kwa upande wake, Balozi Hukka amesema nchi yake kupitia Balozi za Tanzania na Finland zimeanza jitihada za kuandaa utaratibu kwa ajili ya kuwekeza nchini , na kuna  baadhi ya kampuni  tayari ziko   nchini.
Habari hii imetolewa na Ofisi ya mawasiliano ya Waziri Mkuu na Klutwa kwako  na P5 TANZANIA,asante kwa kuwa nami.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA