SERIKALI YATOA MILIONI 999,376,000/= KUGHARIMIA ELIMU BURE MKOANI MWANZA


Na.Issack Gerald-Mwanza.
Serikali  ya awamu  ya Tano chini ya Raisi wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Josefu Magufuri Imetoa kiasi cha shilingi milioni 999,376,000 kwa ajiri ya kughalimia elimu kwa shule za msingi na Sekondari  kwa mwezi januari.

Akizungumza juzi na wakuu wa wilaya , Maafisa Elimu, Na wakurugenzi mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo  amesema kuwa fedha hizo zimetolewa tangu desemba 30 mwaka jana  na kuingizwa kwenye akaunti za shule husika.
Mulongo ameeleza kuwa shule za msingi imeingizwa Milioni 642,648,000 ambazo zimegawanywa kwenye ruzuku za shule, fidia ya ada za wanafunzi, vyakula kwa shule za Bweni na shule za msingi kiasi cha shilingi milioni 356,728,000 na kuwataka wakuu wa shule zote kuepuka ubadhilifu wa aina yoyote wa fedha hizo.
Aidha Bw Mlongo amesema kuwa serikali itaendelea kutoa fedha kila mwezi na kwamba wazazi na  walezi watakao shindwa kuwapeleka watoto wao shule watachukuliwa hatua na kuwajibishwa kisheria.
Asante kwa kuendelea kunifuatilia kwa habari mbalimbali kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA