WAWILI AKIWEMO ASKARI WA JESHI LA POLISI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MWANZA KWA TUHUMA ZA MAUAJI


Na.Issack Gerald-Mwanza
Watu wawili  akiwemo askari wa Jeshi la Polisi wanashikliwa  na jehi la polisi kwa makosa ya mauaji katika maeneo tofauti Mkoani Mwanza.
                                                        
Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza Justus Kamgisha

Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza Justus Kamugisha amesema katika tukio la kwanza,Askari wa Jeshi la Polisi PC F.4965 Joel Francis (41)wa kambi ya polisi Mabatini  wilayani Nyamagana mkoani Mwanza anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji dhidi ya Rafiki yake.
Kamanda wa Polisi Mkaoni humo SACP Justus Kamugisha amemtaja aliyeuwawa kuwa ni Donald Magalata(30)aliyekuwa milinzi wa Mwanza hoteli ambapo amesema,tukio hilo limetokea Januari mosi mwaka huu.
Kamanda Kamugisha ameeleza kuwa PC Francis, januari mosi mwaka huu majira ya saa 7:00 usiku alimfunga pingu miguuni ndani mwake na kumpiga kwa madai kuwa pochi yake  iliyokuwa na vitu vyake haikuonekana na kuhisiwa kuwa aliiba.
Hata hivyo Marehemu alijaribu kuomba msaada kwa majirani ambapo walifika eneo la tukio na kumpeleka hospitali ya Rufaa ya Bugando na kufariki dunia usiku wa kuamkia januari 02 mwaka huu.
Aidha  Kamanda Kamgisha ameeleza kuwa Mtuhumiwa anashikiliwa na polisi na atafikishwa mahakani pindi uchunguzi wa tukio hilo utakapo kamilika.
Wakati huo huo katika tukio la pili,Kamanda Kamgisha amesema,Mwana mme moja mkazi wa Izunge Bwiro wilayani Ukerewe mkoani Mwanza anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji  baada ya kugombania mwanamke katika ukumbi wa disco kijijini humo.
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza SACP Justus Kamugisha amesema kuwa tukio hilo limetokea January 2 mwaka huu majira ya saa 6 usiku na kumhusisha Bw Michael Charles(26) aliyemuua  Ngereja Mashenene(30).
Kamanda Kamugisha ameeleza kuwa Bw Michaele Charles alimchoma kisu kifuani Bw  Ngereja baada ya kugombania mwanamke katika ukumbi wa Disko jina lake limehifadhiwa na baadae akafariki dunia wakati akipelekwa Hospitalini.
Aidha Mtuhumiwa amekamatwa na upelelezi wa shauri hili utakapo kamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo mkabuili.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA