WATATU WAUAWA WILYANI MLELE KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI,LIMO LA BABA NA MWANAWE KULIWA NYAMA NA SIMBA


Na.Issack Gerald-Mlele Katavi
Watu watatu wamekufa katika matukio mawili tofauti Wilayani Mlele Mkoani Katavi likiwemo tukio la baba na mwanae kuliwa na samba jike mzee.
                                         
Baadhi ya Simba katika Hifadhi ya taifa ya wanayama ya Katavi

Katika tukio la kwanza,akithibitisha kutokea kwa tukio hilo,Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo Januari 4 mwaka huu majira ya saa ya saa 3 usiku katika maeneo ya kitongoji cha makaburi wazi kata ya Starike Tarafa ya Nsimbo Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi.
Kidavashari amesema,wawili waliofahamika kwa majina ya  John Jeremiah (41) mkazi wa Matandarani na Patrick John (05) ambaye ni mtoto wa marehemu John Jeremiah wote kwa pamoja waliuawa kwa kushambuliwa vikali na simba jike mzee.
Kamanda Kidavashari amesema,katika tukio hilo,simba huyo alifika katika nyumba ya marehemu ya  John Jeremiah  ambayo ni kambi ya muda kwa ajili ya uangalizi wa mashamba na kuanza kushambulia kuku wawili, ambapo punde aliingia ndani ya kaya ya marehemu John Jeremiah na kumshambulia vibaya sehemu za siri, shingoni na kichwani ambapo licha ya kupiga kelele za kuomba msaada ziliweza kusikika kwa majirani hakupata msaada wa haraka kuokoa maisha yake.
Baada ya hapo simba huyo alimchukua marehemu Patrick John mpaka vichakani na kuanza kumla nyama ambapo Mpaka kufikia alfajiri ya siku ya tukio kabla ya simba huyo kuuawa,alikuwa amembakiza marehemu kichwa na mikono.
Kuhusiana na tukio hilo,Kamanda Kidavashari amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na askari wa wanyama pori TANAPA walifanya msako na kufanikiwa kumkuta simba huyo akiendelea kumla nyama Patrick John ambapo hata hivyo samba huyo aliuawa.
Katika tukio la Pili,mtu mwingine aliyefahamika kwa jina la Heleni Malelemba(40) mkazi wa kitongoji cha Uzumbura aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni na kichwani na watu wasiojulikana.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amesema kuwa tukio hilo,limetokea Januari 4 mwaka huu majira ya saa saba usiku katika kitongoji cha Uzumbura kijiji cha Ikuba, Tarafa ya Mpimbwe, Wilayani Mlele.
Amesema kuwa,siku ya tukio,marehemu alikuwa anaendesha pikipiki aina ya TOYO rangi Nyekundu isiyokuwa na namba za usajili akitokea senta ya usevya kuelekea nyumbani kwake Uzumbura, ambapo akiwa njiani ndipo alipoviziwa na watu wasiojulikana na kufanyiwa mauaji hayo kisha watuhimiwa kutokomea kusikojulikana pasipo kuchukua pikipiki ya marehemu.
Chanzo cha tukio hili bado hakijafahamika na upelelezi unaendelea kwa kushirikiana na wakazi wa eneo la Tarafa ya Mpimbwe ili kubaini sababu iliyopelekea mauaji haya ambapo Mpaka sasa hakuna watu walioshukiwa na kukamatwa kuhusiana na tukio hili ili sheria iweze kuchukua mkondo kwa wahusika wote.
Kufuatia matukio hayo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi anatoa wito kwa wananchi hasa wakulima na wafugaji ambao shughuli zao huzifanya au hutegemea porini au mazingira karibu na mbuga za wanyama,kuzingatia usalama wao kwanza kwa kuhakikisha wanakuwa makazi imara na salama dhidi ya wanyama wakali wa porini.Pia, anaendelea kuwaonya watu wanaopenda kujichukulia sheria mikononi kuwa hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi yao.
Asante kwa kuendelea kuwa namii,endelea kuhabarika na P5 TANZANIA

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA