UELEWA MDOGO WA WATU WAISHIO NA VIRUSI VYA UKIMWI,BADO CHANGAMOTO KUUDHIBITI UGONJWA WA UKIMWI


Na.Issack Gerald-Mwanza
Muuguzi wa Kituo kinacho toa huduma kwa watu wanaoishi na maambukizi ya Virus Vya UKIMWI na Yatima Shalom Care House Jijini Mwanza  Bi Edna Evarist amesema uelewa mdogo  wa watu wanaoishi Na VVU ni changamoto katika kudhibiti UKIMWI nchini.
Bi Evaristi ameyasema hayo wakati  akizungumza na Redio Kwizera Juu ya kauli mbiu ya taifa chini ya wizara ya afya na usitawi wa jamii kufikia sufuri tatu  katika kudhibiti maambukizi mapya ya VVU, vifo vitokanavyo na VVU Na unyanyapaa.
Amesema kuwa watu wenye virusi vya UKIMWI wengi wao wamekuwa wakiendeleza maambukizi hayo kwa kuoa na kuolewa au kuanziasha mahusiano mapya bila kuwahusisha wenzi wao huku wakijua hali zao kiafya na kusababisha maambukizi  ya UKIMWI nchini kuendelea.
Aidha mratibu wa kituo hicho Bw Msafiri Wana amesema kuwa Idadi ya watoto yatima kutokana na vifo vianavyo sababishwa na Ukimwi imepungua baada ya jamii kujua umuhimu wa matumizi sahihi ya dawa za punguza  makali ya VVU.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA