UJENZI WA BARABARA KIWANGO CHA LAMI KUTOKA MPANDA HADI SUMBAWANGA KUKAMILIKA 2016


Na. Issack Gerald -Dodoma
SERIKALI imesema ujenzi wa barabara ya Mpanda hadi Sumbawanga kwa kiwango cha lami unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2016.
                                                     
Bungeni Dodoma

                                                     
Jengo linalotumika katika vikao vya bunge Mjini Dodoma

Naibu waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani amesema hayo leo bungeni mjini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalum Bi. Anna Lupembe aliyetaka kujua ujenzi wa barabara hiyo utakamilika lini.
Naibu waziri Ngonyani amesema ujenzi wa barabara ya Sumbawanga hadi Mpanda umegawanyika katika sehemu nne, ambazo ni Sumbawanga kanazi kilometa 75, Kanazi-Kibaoni Kilometa 76. 6, Kibaoni- Stalike kilometa 72 na Stalike-Mpanda kilometa 36.
Amesema upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa sehemu iliyobaki ya Kibaoni hadi Stalike umekamilika na serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi .

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA