AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPATA KIPIGO KIKALI-P5 TANZANIA MEDIA INAKUSOGEZEA HIYO


Na.Issack Gerald-Mlele
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Ramadhani Ally (20), mkazi wa Kalovya Inyonga,amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya Inyonga kufuatia kipigo kikali alichokipata toka kwa Ntemwa Kabembenya(26) mkazi wa Ipwaga.

Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri kidavashari,amesema kuwa tukio hilo limetokea  tarehe 23.01.2016.
Kabla ya marehemu kufariki,Marehemu alikuwa amesimama na dada wa mtuhumiwa aliyejulikana kwa jina la Ngoro Mbogo (12) mkazi wa Ipwaga ambapo baada ya mtuhumiwa kuwakuta wakiwa wamesimama pamoja huku wanaongea kitendo kile kilimkasirisha mtuhumiwa ndipo alipoanza kumshambulia kwa kumpiga kwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake.
Kamanda Kidavashari amesema, marehemu alifariki dunia baada ya kupelekwa  katika hospitali ya Wilaya Mlele kwa matibabu baada ya kipigo alichokipata tarehe 22.01.2016 Chanzo cha tukio hili ni ugomvi kati ya marehemu na mtuhumiwa ambapo hata hivyo Jeshi la Polisi linamshikilia mtuhumiwa Ntemwa Kabembenya(26) na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA