MAMA AMUUA MTOTO WAKE AMFUNGA KAMBA SHINGONI AMTUNDIKA JUU YA MWEMBE MPANDA.


Na.Issack Gerald-Katavi
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi linamshikilia Sado Roket (26) mkazi wa Mnyakasi kwa kumuua mtoto wake Nchambi Tungu (11) mkazi wa Mnyakasi  kwa kumpiga kwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo,Kamnda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo tarehe 23.01.2016 majira ya saa 19:50 katika Kitongoji cha Mnyakasi Kijiji cha Ikuba Kata ya Ikuba Tarafa ya Mpimbwe Wilayani Mlele Mkoani Katavi.
Kamanda Kidavashari amesema kuwa mtuhumiwa alimpatia marehemu nguo ili azifue lakini hakuweza kufanya hivyo na ndipo mtuhumiwa alipoamua kuchukua fimbo na kuanza kumpiga kwa kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake mpaka kupelekea kifo chake.
Baada ya kutekeleza azima yake mtuhumiwa alimchukua marehemu na kumpandisha juu ya mti wa mwembe na kumfunga kwa kamba shingoni na kumwacha akining`inia ili ionekena kuwa marehemu alijinyonga.
Chanzo cha tukio hili ni marehemu kushindwa kufua nguo za mama yake mzazi kisha kumpiga na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake mpaka kufariki.
Hata hivyo Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika ili kujibu tuhuma inayomkabili.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi anatoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi kwani ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za haki za binadamu za kuishi na ni kinyume cha maadili ya kijamii badala yake wawe mstari wa mbele kutii na kuzingatia mwenendo wa sheria za Nchi katika masuala mbalimbali.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA