VIKUNDI 14 VYA WAJASILIAMALI 60 MPANDA WAKOPESHWA MILIONI 27


Na.Agness Mnubi-MPANDA.
WAJASIRIAMALI  60  sawa na  vikundi 14 kutoka Wilayani Mpanda na Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamepata mkopo wa sh. Million 27 kupitia Mfuko wa Wajasiriamali Mpanda(METF).

Akikabidhi hundi za mikopo kwa wajasiriamali hao katika ukumbi wa kanisa  katoliki leo, Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, katibu tawala Bw. Donald Nkoswe Nkoswe amewataka kutumia fedha hizo kwa usahihi na kurudisha ili ziwanufaishe na watu wengine.
Katibu wa Mfuko huo wa  Wajasiriamali Mpanda Bi. Zena Kapama amewataka  kutumia fedha hizo kwa usahihi ili kukuza mitaji ya biashara zao, na  kuweza kulipa riba kwani   wanarejesha kila mwezi kwa riba ya asilimia 15 kwa mwaka
Mfuko wa wajasiriamali Mpanda ulianzishwa tareher 4/1/2009 na aliyekuwa waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania MIZENGO PINDA  kwa kuwakutanisha wafanyabiashara kwa lengo la kuanzisha mfuko ambao utawawezesha wajasiriamali wadogo   kukopa kwa masharti na kwa riba nafuu.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA