MADIWANI NSIMBO WATAKIWA KUSIMAMIA SHUGHULI ZA MAENDELEO


Na.Issack Gerald-NSIMBO
Baraza la madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi, limetakiwa kusimamia kikamilifu shughuli za maendeleo katika kata zao pamoja na kutunza siri za serikali.

Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Mlele kanali mstaafu Issa Suleiman Njiku katika zoezi la kuwaapisha madiwani hao katika ukumbi wa halmashauri wilaya ya Nsimbo.
Kanali Njiku amesema diwani anapaswa kusimamia miradi mbalimbali  pamoja na kusimamia hifadhi na mapori tengefu, ili kuzilinda maliasili kwa ustawi wa taifa la Tanzania.
Aidha madiwani hao baada ya kuapishwa wameteua kamati mbalimbali zitakazosimamia maendeleo katika halmashauri hiyo, pamoja na kumchagua diwani wa kata ya Machimboni Bw. Raphael Kalinga kuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA