MADIWANI MPANDA WATAKIWA KUWAJIBIKA KWA WANANCHI


Na.Issack Gerald-MPANDA.
MADIWANI wanaounda baraza la madiwani halmashauri wa wilaya ya mpanda walioapishwa leo wametakiwa kuanza kazi kwa kuzingatia maadili na kuacha kufuata itikadi ya vyama vyao ili kuleta maendeleo ya wananchi kwaujumla.

Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dk.Ibrahim Msengi katika ukumbi wa idara ya maji katika zoezi la kuwapisha madiwani hao.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bw. Pazza Mwamlima amewataka madiwani hao kufanya kazi walizoagizwa na wananchi na kutatua changamoto zilizopo katika kata zao ikiwemo elimu na afya.
Nao baadhi ya madiwani walioapishwa wamesema watafanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa, na kufuata kasi aliyoanza nayo Rais wa serikali ya awamu ya tano Dk.John Pombe Magufuli.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA