ASKARI 38 WA WANYAMA PORI WATUNUKIWA VYETI KATAVI


Na.Issack Gerald-MPANDA
Jumla ya wahitimu 38 walioshiriki mafunzo awamu ya pili ya Kijeshi katika Hifadhi ya Wanyama pori Katavi, wametunukiwa vyeti katika madaraja mbalimbali.

Akifunga mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa hifadhi za taifa Nchini Bw. Matongo Mtahiko amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuimarisha nidhamu ya kuwawezesha wahitimu kujua matumizi sahihi ya silaha.
Aidha Bw. Mtahiko amesema mafunzo hayo ni maandalizi ya shirika la hifadhi Nchini kutoka katika mfumo wa kiraia kwenda katika mfumo wa jeshi Usu.
Katika mafunzo hayo idadi ya wanawake waliohitimu ni wanane wakati wanaume ni thelathini.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA