HAKI ZA BINADAMU WACHARUKA KUHUSU UKATIRI UNAOENDELEA MKOANI KATAVI


Na.Issack Gerald-Mpanda
Wananchi Mkoani Katavi wametakiwa kuripoti matukio ya ukiukwaji  wa haki za binadamu katika Ofisi za haki za binadamu wanapoona mamlaka husika Mkoani hapa zinawanyanyasa katika haki zao mbalimbali.

Unapozungumzia haki za binadamu,unakuwa unazungumzia kuhakikisha kuwa haki za msingi kwa binadamu zinapatikana kwa haki tena ikiwezekana kwa mjibu wa sheria.
Siku ya haki za binadamu ilianzia nchini Marekani wakati waafrika weusi nchini Humo walipokuwa wakidai haki zao ili kujikomboa kutoka katika minyororo ya wazungu ambapo pia mbali na Afrika pia hata Nchi ya Waisreal walipokuwa wamfungwa kule marekani walifanya hivyo ili kunijinasua na matukio kandamizi.
Miongoni mwa haki za binadamu ni pamoja nahaki ya kuishi.Lakini kwa mara kadhaa tuhuma mbalimbali zimekuwa zikisikika maeneo mbalimbali ya dunia kuwa uvunjifu wa haki za binadamu umekithiri ambapo mashirika kama Amnesty International yanayotetea haki mbali mbalimbali za binadamu yamekuwa yakiingilia kati yanapogundua viashiria au vitendo vya uvunjifu wa amani.
Katika kuangazia siku ya haki za binadamu inayoadhimishwa kila ifikapo Desema 10,nimemtafuta Stanslaus Michael Kisesa  Mratibu wa Haki za Binadamu Mkoani Katavi na Ukanda wa Mikoa ya Magharibi kwa ujumla ambapo katika mahojiano na P5 TANZANIA MEDIA pamoja na mabo mengine amesema kuwa Wananchi Mkoani Katavi wanatakiwa kuripoti matukio ya ukiukwaji  wa haki za binadamu katika Ofisi za haki za binadamu wanapoona mamlaka husika Mkoani Katavi zinawanyanyasa katika haki zao mbalimbali pale ambapo wahusika kwa maana wanaotakiwa kutoa huduma kwa mjibu wa sheria wanazikiuka maksudi kwa lengo la maslahi binafsi.
Florance  Chareles ni mmoja wa wakazi waliopo mtaa wa Mpanda Hotel Manispaa ya Mpana Mkoani Katavi kwa, upande wake akizungumzia siku ya haki za binadamu ambapo pamoja na kuzungumza mengi anaona elimu bado haijatolewa kwa kiasi cha kutosha kuwapelekea raia kutambua jinsi ya kupambana na viashiria vya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Sekta mbalimbali zikiwemo za ardhi na maliasili zimekuwa zikitajwa na wananchi Mkoani Katavi zikihusishwa na matukio au vitendo vya unyanyasaji kwa baadhi ya watu wakati mwingine hadi kupelekea vifo.
Aidha mratibu wa haki za binadamu Mkoani Katavi na Ukanda wa Magharibi kwa ujumla unaojumisha mikoa ya Rukwa,Katavi,Kigoma na Tabora anazungtumzia ametaja idara ambazo wamekuwa wakizishughulika nazo katika utatuzi wa matatizo ya wananchi hususani katika idara ya ardhi Manispaa ya Mpanda  ambapo amesema wamefanikiwa kuwaelekeza hatua za kisheria katika kudai haki yao na hatimaye kupata haki yao.
Naye Emmanuel Mgiuna kwa upande wake,ni mwanafunzi wa anayesomea sheria ya haki za Binadamu Mkoani Katavi amewaomba wakurugenzi katika Halmashauri za Wilaya Mkoani Katavi kuhakikisha wanazingatia sheria ili kila raia apate haki yake katika masuala mbalimbali kwa mjibu wa sheria.
Hata hivyo Kisesa ametoa wito kwa watumishi wa umma,na waliopo katika vitengo vya sheria wakiwemo mawakiri binafsi kutojihusisha vitendo vya kutoa na kupokea na rushwa na badala yake watende haki kwa kila raia kama sheria zinavyoelekeza katika mambo wanayoyahitaji raia.
Baadhi ya maeneo ambayo wakazi wamekuwa wakilalamika kudai haki zao ni pamoja na Kijiji cha Luhafwe ambako inaadiwa mwaka 2013 kulitokea ukiukaji wa haki za binadamu ambapo mpaka leo wananchi hawajafahamu uhalali wa kijiji chao kuwepo licha ya kuwa na huduma za jamii ikiwemo shule.
Maeneo mengine ni pamoja na Sitalike  Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ambapo wananchi wamekuwa wakidai kupigwa na askari wa wanayama pori mara kadhaa wananchi wakitumiwa kuvamia hifadhi ya Taifa ya Wanyama Katavi lakini pia suala la viwanja hususani Maeneo ya Mtaa wa Nsemulwa kata ya Nsemulwa Manispaa ya Mpanda likionekana kuwa sugu kwa kushindikana kupatiwa ufumbuzi wa kutosha tangu mwaka 2013.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA