CHANAGAMOTO ZAENDELEA KUIANDAMA SHULE YA MSINGI KAWANZIGE


Na.Issack Gerald-MPANDA.
SHULE ya Msingi Kawanzige iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi yenye jumla ya wanafunzi 663 inakabiliwa na upungufu wa madarasa ya wanafunzi pamoja na ofisi za Walimu.

Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Shuleni hapo,Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Kawanzige Ajaye Patrick amesema Wanafunzi hubadilishana madarasa wakati wa kusoma kwa muda hali inayosababisha usumbufu kwa wanafunzi. 
Mwalimu huyo ameiomba  Serikali kujenga madarasa na ofisi za walimu, huku akisema kuwa wazazi na wanafaunzi wameonesha ushirikiano mkubwa katika kujenga shule hiyo hususani ufyatuaji wa tofali.
Sambamaba na Changamoto zinazoikabili shule hiyo bado inafanya vizuri katika mitihani ya Kitaifa ambapo mwaka jana ilikuwa ya kwanza kati ya Shule 26 zilizopo Manispaa ya Mpanda ambapo kwa  mwaka huu imeshika nafasi ya nne  ikiwa na ufaulu wa asilimia 100.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA