WANAFUNZI WAOMBA KUENDELEZWA ELIMU

Wanafunzi wakiwa darasani Shule ya msini Mpanda iliyopo Manispaa ya Mpanda

NA.Issack Gerald-Mpanda
Wanafunzi wa shule ya msingi Mpanda  iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamewaomba wazazi na walezi kuwaendeleza kielimu wanapokuwa wamehitimu masomo ya darasa la saba na kufaulu kujiunga na kidato cha kwanza.

Wanafunzi hao wakihojiana na P5 TANZANIA wamesema kuwa  sababu kuwa inayowafanya wasiendelee kielimu ni mwamko mdogo wa kielimu katika jamii.
Kwa upande wa mwalimu  mkuu wa shule hiyo Bw Razaro Jangu amesema wamefanya maandalizi ya kutosha ili kuhakikisha wanafunzi wote wanafaulu kwa kiwango cha juu.

Aidha Mwl Jangu amekiri  kuwepo kwa tatizo la wazazi walio wengi kuwa na mwamko mdogo kielimu jambo linalo kwamisha ndoto za wanafunzi hao kutokana na wanafunzi hao kutofikia ngazi ya juu kielimu kutokana na kutelekezwa na wazazi wao sababu kubwa ikitajwa ni umaskini na mwamko mdogo wa elimu.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA