CHADEMA WAPINGA TAMKO LA POLISI VIKUNDI VYA ULINZI NDANI YA VYAMA VYA SIASA ,CCM WAKUBALI

Na.Issack Gerald-MPANDA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Wilayani Mpanda Mkoani Katavi kimepinga kauli ya jeshi la Polisi Mkoani hapa kupiga marufuku vikundi vya ulinzi katika vyama vya siasa wakati wa kampeni na uchaguzi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama hicho Wilayani Mpanda Abraham Mapunda wakati akihojiana na Mpanda Radio  katika ofisi za chama hicho kuhusu agizo la jeshi la polisi kutupilia mbali vikundi vya ulinzi ndani ya chama.
Akimezungumza Na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilayani  Mpanda Bw.Beda Katani kuhusiana na tamko la jeshi la polisi ambapo pamoja na mambo mengine amesema anaunga mkono jeshi la Polisi kupiga marufuku vikundi vya ulinzi ndani ya vyama vya siasa ili kuimarisha usalama.
Wakati huohuo baadhi ya wakazi Manispaa ya Mpanda wakizungumza na Mpanda Radio mbali na kusema mengi wamelitaka jeshi la polisi kusimamia sheria na maadili ya kazi zao katika ulinzi na kutenda haki kwa vyama vyote  vya siasa wakati wa kampeni na Uchaguzi.
Kauli za viongozi wa vyama na maoni ya wananchi kuhusu vikundi vya ulinzi katika vyama vya siasa zimekuja ikiwa ni siku moja baada ya Mratibu mwandamizi na mnadhimu wa jeshi la polisi Mkoani KATAVI  Focus Malengo kutoa tamko hilo kupitia Kipindi cha Polisi Jamii kilichorushwa na Mpanda Radio Alhamisi saa kumi jioni.

Kikundi cha ulinzi cha Chadema kinaitwa Red Briged wakati kile cha CCM kinaitwa Green guard.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA