WANAFUNZI 11 WAPATA MIMBA KATAVI

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Michael Francis Nzyungu amesema wanafunzi wapatao 11 katika shule zake wamepata ujauzito na kukatiza kuendelea na masomo katika kipindi cha mwaka 2017.
Nzyungu ameibainisha hali hiyo juzi wakati akiwasilisha taarifa kwa mkuu wa Mkoa wa Katavi kupitia kikao cha wadau wa elimu kilichokuwa kimeandaliwa maalumu ili kujadili na kutathmini hali ya ufaulu wa wanafunzi Mkoani Katavi katika mitihani ya taifa kwa shule za msingi na sekondari.
Amesema kati ya mimba hizo 11 zilizoripotiwa kwa katibu tawala wa Mkoa wa Katavi,mimba 3 zimeshafikishwa polisi huku mimba nyingine zikishughulikiwa katika ngazi ya maafisa watendaji wa kata na mitaa ili kutafuta ufumbuzi.
Kwa upande wao wanafunzi akiwemo Paulina Wilison wa Mpanda Girls Sekondari,na Philbeti Mapunda mwenyekiti wa kamati ya shule ya sekondari Shanwe ambaye pia alikuwa miongoni mwa wadau wa elimu malezi mabaya,umaskini pamoja na ukosefu wa mabweni hasa kwa watoto wa kike bado ni vyanzo vikubwa vinavyochangia mimba kwa wanafunzi walio katika umri mdogo.
Hata hivyo serikali imekuwa ikiagiza kuchukuliwa hatua kali za kisheria dhidi ya wanaosababisha mimba kwa wazazi pamoja na wazazi au walezi wanaowaoza watoto wao kwa kigezo cha kupata mahali.
Mkoa wa Katavi ndiyo unaoongoza kwa mimba za utotoni kati ya mikoa ya Tanzania kwa kuwa na asilimia 45 ambapo wengi wao wanakuwa katika umri wa kuwa shuleni.
Habari zaidio ni www.p5tanzania.blogspot.com 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA