RAIS MAGUFULI ATUMBUA MKURUGENZI


Rais Dkt.John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpwapwa mkoani Dodoma,Mohamed Maja kuanzia leo kutokana na kushindwa kusimamia ukusanyaji wa mapato na kuisababishia halmashauri hiyo upotevu mkubwa wa fedha za serikali.
Hayo yamebainishwa na Katibu mkuu wa ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Tamisemi Mussa Iyombe wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma.
Amesema utenguzi huo umefanyika ili kutoa nafasi ya kufanyika uchunguzi juu ya tuhuma hizo.
Iyombe amesema tume iliyoundwa kufanya uchunguzi wa utendaji katika ofisi ya mkurugenzi huyo imebaini baadhi ya fedha zinapotea mikononi mwa watu na mkurugenzi huyo kushindwa kudhibiti.
Wakati huo huo Iyombe amesema Mkurugebnzi huyo kwa sasa yupo chini ya uchunguzi.
Kwa upande wake,Naibu Waziri wa Tamisemi Josephat Kandege, amewataka wenyeviti wa halmashauri kote nchini kuzingatia mafunzo waliyopewa na uongozi wa chuo cha serikali za mitaa hombolo ili wawe mabalozi bora katika maeneo yao.
Habari zaidio ni www.p5tanzania.blogspot.com 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA