HALMASHAURI YA WILAYA MPANDA KUWAWEZESHA WATU WENYE ULEMAVU MWAKA FEDHA 2018/2019

Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imesema kuanzia bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 itaanza kutoa asilimia 2 ya mikopo kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
Hatua hiyo imebainishwa na Kaimu Mkurugenzi  halmashauri hiyo Samson Medda ambapo amesema katika mgawanyo wa asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri wanawake watakuwa wanapata asilimia 4 na vijana asilimia 4 na 2 kwa watu wenye ulemavu.
Kwa mjibu wa Medda,mpaka kufikia mwezi machi mwaka huu,halmashauri imetoa fedha kutoka katika mapato ya ndani  kiasi cha shilingi milioni 119 kwa ajili ya kuwezesha vikundi vya wanawake  na vijana.
MAENEO AMBAYO HALMASHAURI ILIWEZESHA
1.Kikundi cha vijana Kata ya Majalila cha kufyatua tofali kilipewa pesa
2.Kikundi cha wanawake cha Sibwesa kinachoseketa mashuka na vikoi kilipewa fedha
3.Mashine ya kukoboa na kusaga mahindi-kata ya Kabungu
4.Kiwanda cha Chaki na Sabuni-kata ya Ifukutwa
5.Pikipiki 11 zilinunuliwa na kusambazwa vijana ambapo 4-zilipelekwa kwa vijana wa Kata ya mpanda Ndogo,2-kata ya Kapalamsenga,5-kata ya Majalila.
6.Mashine ya kukoboa Mpunga-kata ya Sibwesa
7.Sakosi ya Akina mama inayojumuisha wanawake kutoka Katumba,Sibwesa & Kasekese-walipewa Shilingi milioni 30.
Aidha ametoa wito kwa idara za  maendeleo ya jamii kutoa elimu ya kutosha  kwa wanawake na vijana wajiunge katika vikundi  ili wanufaike na asilimia 10 inayotengwa na halmashauri.
Hata hivyo amesema bado kuna changamoto ya urejeshaji wa fedha wanazozikopesha kwa vikundi mbaimbali vya wajasiliamali.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA