RAIS MAGUFULI ATOA SAA 24 KWA IGP AKIZINDUA NYUMBA 31 ZA POLISI


Rais Dkt.John Magufuli amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP),Simon Sirro kuhakikisha inapofika kesho Aprili 8, 2018 awe ameshawaingiza askari Polisi walionguliwa nyumba zao hapo awali katika nyumba mpya ambazo zimezinduliwa hii leo.
Dkt.Magufuli ametoa agizo hilo leo wakati alipokuwa anazungumza muda mchache alipomaliza kuzindua nyumba za askari zilizojengwa mkoani Arusha.
Amesema anawapa pole kwa majanga yaliyotokea ya kuunguliwa moto,huku akiwapongeza wadau mbalimbali waliojitolea kwa mioyo yao katika ujenzi wa nyumba hizo.
Aidha amesema anataka wale wale walionguliwa ndio waingie humo katika nyumba hizo ambapo ameeleza kuwa nyumba kuugua imedhihirisha makazi ya nyumba za polisi yalivyokuwa mabovu.
Jumla ya nyumba 31 za polisi  mjini Arusha zimezinduliwa tayari kwa ajili ya polisi.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA