KATAVI WAFANYA USAFI WAADHIMISHA KIFO CHA KARUME


Serikali ya Mkoa wa Katavi umefanya zoezi la usafi kama sehemu ya kuadhimisha miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.
Katika taarifa iliyokuwa imetolewa jana na Afisa Habari wa Manispaa ya Mpanda Pius Donald alikuwa amebainisha maeneo yanayofanyiwa usafi kuwa ni pamoja na maeneo ya hospitali,sokoni na stendi kuu.
Serikali imekuwa ikiwataka watanzania kufanya usafi wa hali ya juu katika maeneo yao ili kuendelea kuwa salama ikiwemo kuepuka maambukizi ya magonjwa ya mlipuko kama kipindipindu ambapo imekuwa ikifikia hatua ya kuchukua hatua kali za kisheria wa watu wanaokaidi kufanya usafi katika maeneo yao.
Hayati Sheikh Abeid Amani Karume alizaliwa mwaka 1905 na alifariki dunia tarehe 7 Aprili 1972 kwa kupigwa risasi hadaharani wakati akicheza bao huko Zanzibar.
Habari zaidio ni www.p5tanzania.blogspot.com 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA