AJALI YA BODABODA NA GARI KATAVI

Dereva wa pikipiki maarufu kama Boda boda ambaye  jina lake halikufahamika Mara Moja Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,amejeruhiwa baada ya pikipiki yenye namba za usajil Mc 743 BQG aliyokuwa akiendesha kuligonga kwa Nyuma gari aina ya Raum eneo la Buzogwe njia mbili.
Mashuhuda wa tukio hilo  ambalo limetokea leo wamesema,dereva huyo alikuwa akijaribu kuingia barabara kuu ya Buzogwe ndipo akawa amegongana na  Gari lenye namba za usajili T498 CFU. 
Kwa mjibu wa mashuhuda hao,madereva wote wawili walikuwa na makosa baada ya wote kutozingatia sheria za usalama barabarani.
Hata hivyo dereva wa gari hilo ambalo limegongana na pikpiki ametokomea kusikojulikana baada ya kutoonekana eneo la tukio baada ya Ajali hiyo kutokea.
Hata hivyo askari polisi wa usalama barabarani ambao walifika eneo la tukio,wamekataa kuzungumzia tukio hilo wakidai wao siyo wasemaji.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA