ZANZIBAR YAPAA MAAMBUZI YA KIFUA KIKUU


Wizara ya Afya Zanzibar imesema kasi ya Ugonjwa wa kifua kikuu imekuwa ikiengezeka kwa kiwango kikubwa ambapo  katika mwaka 2017 jumla ya wagonjwa 948 waligundulika kuwa na ugonjwa huo.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na siku ya kifua kikuu katika ukumbi Wizara hiyo Mnazi mmoja Mjini Zanzibar ,Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Muhammed amesema Ongezeko hilo limefikia idadi ya wagonjwa 225 ikilinganishwa na mwaka 2016.
Amesema kutokana na ongezeko hilo Utafiti unaonesha bado Zanzibar inakabiliwa na tatizo la Uelewa mdogo juu ya Maradhi hayo jambo ambalo linapelekea wananchi kushindwa kuhudhuria katika vituo kwa wakati ili kupunguza maambukizi.
Amesema  kutokana na Ugonjwa wa kifua kikuu kuwa ni ugonjwa wa tisa unaosababisha vifo kwa wagonjwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha inachukuwa jitihada mbalimbali ikiwemo  kuendelea kutoa elimu ya kujiepusha na viashiria vya maradhi hayo.
Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Afya ulimwenguni takwimu zinaonesha kuwa kwa Tanzania ni nchi ya 30 ulimwenguni zenye idadi kubwa ya wagonjwa wa kifua kikuu ambapo kwa mwaka 2016 jumla ya watu milllioni 10.4 wameugua ugonjwa huo kati yao wagonjwa Millioni 1.6 walifariki dunia.
Aidha Waziri Hamadi ametowa wito kwa Viongozi wa serikali ,Wadini na Siasa kutumia nafasi walizonazo katika taasisi zao na Mkutano kutoa elimu juu ya Ugonjwa wa maradhi ya kifuua kikuu ili kupunguza tatizo la uhaba wa elimu katika jamii.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo shirikishi cha Homa ya Inni,kifua na Ukoma  Farhat Khalid amesema ni vyema kwa wananchi kuachana na visababishi vya Maradhi ya kifua kikuu ikiwemo Ulevi na uvutaji sigara ili kutokomeza ugonjwa huo Nchini.
Aidha ametowa wito kwa jamii kufika katika vituo vya afya baada ya kujigundua kuwa wanadalili za Ugonjwa huo ili waweze kunufaika na huduma za matibabu kwa wakati.
Siku ya kifua kikuu huadhimisha kila ifikapo March24 ambapo kwa mwaka huu siku hiyo inatarajiwa kuadhimishwa katika ukumbi wa baraza la wawakilishi la Zamani Mjini Unguja ikiwa na ujumbe Usemao ‘TUNAHITAJI VIONGOZI MAHIRI WA KUONGOZA MAPAMBANO YA KUMALIZA KIFUA KIKUU’’.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA