KAULI YA WAZIRI ISIPOFAFANULIWA VIZURI INAWEZA KUSABABISHA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU SHULENI

Miaka michache baada ya serikali yenyewe kufuta adhabu ya viboko shuleni,Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Dk.Mwigulu Nchemba,amewataka walimu kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi kwa kuwafundisha maadili mema na na inapobidi matumizi ya fimbo yatumike.
Waziri Nchemba ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika harambee ya ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari  Lulumba Wilayani Iramba mkoani Singida ambapo amesema walimu wanatumia fimbo kunyoosha nidhamu za wanafunzi ili kutengeneza hatma ya nchi.
Katika hatua nyingine amesisitiza kuwa ni lazima kuendelea kulinda hadhi za walimu kwa kuwapatia miundombinu bora ya ofisi na vyumba vya madarasa.
Mbali na hayo Dk.Nchemba amesema majengo ya taasisi za serikali yanapaswa kuwa bora zaidi na sio kutumia ramani za awali pekee kwani zinapaswa kuboreshwa kulingana na maendeleo yaliyopo.
Imekuwa ikishuhudiwa baadhi ya walimu wakiwachapa wanafunzi mpaka kusababisha majeraha hata baadhi ya walimu hao kufukuzwa kazi,je,kauli ya Waziri Mwigulu inakuwaje?
Chanzo:Eatv/Mpekuzi Blog

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA