BARAZA LA MAASKOFU KUTEMA CHECHE KESHO KUHUSU HALI YA USALAMA WA TANZANIA NA WATU WAKE


Baraza la maaskofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri chini Tanzania (KKKT) linasema umoja na amani ya Tanzania viko hatarini.
Katika waraka wa ujumbe wa pasaka unaosambaa katika mitandao ya kijamii na kutarajiwa kusomwa kesho katika makanisa mbali mbali ya KKKT nchini Tanzania, baraza hilo limeorodhesha mambo kadhaa ambayo wameyataja kuwa ndio tishio la umoja na amani ya nchi hiyo.
Waraka umeyataja baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na utekaji,utesaji,kupotea kwa watu, mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa,mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi,vitisho, ubambikiziaji wa kesi na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi.
Waraka umeongeza pia kwamba uhuru wa kujieleza,kutoa na kupokea habari umeendelea kutoweka nchini huku ukionya kubanwa na hatimaye kuelekea kupungua kwa uhuru wa Bunge,Mahakama, na Tume ya Uchaguzi, ukisema hatua hii ni pamoja na kudhoofishwa kwa serikali za Mitaa.
jumbe huu kutoka baraza la maaskofu wa KKKT umekuja siku chache tu baada ya ujumbe wa Kwaresima uliotolewa na baraza la Maaskofu wa kanisa Katoliki
Maaskofu wa Katoliki waligusia pia kuminywa kwa uhuru wa kutoa na kupokea habari huku wakitaja baadhi ya vyombo vya habari kufungiwa au kusimamishwa kwa muda.
Walionya kwamba katika mazingira haya ni rahisi kwa jamii kufarakana na hata kujenga chuki kiasi cha kuhatarisha amani, usalama na hadhi ya uhai wa binadamu.
Maaskofu wa KKKT wameasa kwamba roho iliyokuwemo kwa waasisi wa taifa na hata kusaidia kupata uhuru mwaka 1961 bila kumwaga damu,inapaswa kuendelea wakati wote.
Habari zaidi ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM  

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA