MWENYEKITI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO AFAFANUA UKOSEFU WA DIWANI KATA YA KATUMBA

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi Mh.Raphael Kalinga amesema tayari ametoa taarifa kwa katibu mkuu kuarifu kuhusu Kata ya Katumba katika halmashauri hiyo kutokuwa na Diwani tangu mwaka jana.

Akizungumza mapema leo amesema halmashauri inajipanga kwenda katika kata hiyo ili kukutana na watendaji wakiwemo wananchi ili waendelee kutoa ushirikiano kwa diwani wa viti maalumu.

Katika hatua nyingine amesema wanasubiri maelekezo kutoka ngazi za juu kujua hatima ya suala hilo.

Siku ya jana Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Mh.Rhoda Kunchela amesema kitendo cha wananchi wa kata hiyo kukosa Diwani hakikubaliki kwani kinadhoofisha jitihada za maendeleo  ya wananchi.
Diwani wa kata hiyo Seneta Baraka alifungwa mwaka jana miaka 3 jera  kwa kosa la kupokea rushwa kwa mfugaji wa kata hiyo ili amuidhinishie eneo la kufugia ambalo limepigwa marufuku na Mahakama.


Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA