AJALI YAU 11 YAJERUHI WENGINE MKOANI KAGERA

Watu 11 wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa kutokana na ajali ya gari aina ya Hiace kugongana na malori matatu katika kijiji cha Mubigera wilayani Biharamulo mkoani Kagera usiku wa kuamkia.

Gari hiyo yenye namba za usajil T.542 DKE ilikuwa ikitokea Wilayani Kibondo kuelekea Kahama mkoani Shinyanga huku maroli yaliyohusika kwenye ajali hiyo yakiwa  chini ya usalama wa jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Agustino Olomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na idadi hiyo ya vifo na kwamba taarifa zaidi na majina itatolewa baada ya muda mfupi ili kutambua majina ya waliopoteza maisha

Naye Mganga Mkuu wa hospitali teule ya Biharamulo Dr.Grasmus Sebuyoya amethibitisha kupokea miili ya watu hao wakiwa maiti na majeruhi sita na kwamba kati ya majeruhi hao wawili hali zao ni mbaya na waliofariki wa jinsia ya kiume ni saba na jinsia ya kike ni watatu


Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA