LOWASSA AANIKA ALICHOZUNGUMZA NA RAIS MAGUFULI IKULU

Mjumbe wa kamati kuu ya chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania,CHADEMA, Edward Lowassa amefichua kuwa Rais John Magufuli alimuomba arejee chama tawala cha CCM wakati wa mazungumzo yao juma lililopita.


Lowassa na Magufuli walikutana Ikulu kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi wa 2015Katika 

Haki miliki ya pichaIKULU
Image caption

Lowassa na Magufuli walikutana Ikulu kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi wa 2015 taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Chama cha Demokrasia na Maendeleo,imenuukuu ujumbe wa Lowasa ukieleza kuwa  Rais Magufuli alimshawishi arudi na kujiunga na CCM jambo ambalo hakukubaliana nalo.

Wiki iliyopita,kiongozi huyo wa upinzani nchini ambaye pia ni Waziri mkuu wa zamani, amekutana na Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli Ikulu na kumsifu sana kwa kazi anayoifanya.

Lowassa aliwania urais kupitia chama kikuu  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015 lakini akashindwa na Dkt Magufuli aliyewania kupitia Chama cha Mapinduzi.


Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA